Yaliyo semwa na Marjaa Dini mkuu: ni wazi kua kufuata njia za amani ndio sharti kubwa la kufanikiwa katika vita ya islahi.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza umuhimu wa kufuata njia za amani katika maandamano, akasema kua ndio sharti kubwa la mafanikio, aidha amesifu asilimia kubwa ya watu wanaofanya maandamano ya amani.

Ameyasema hayo katika khutuba ya swala ya Ijumaa (16 Rabiul-Aakhar 1441h) sawa na (13 Desemba 2019m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo: (Enyi wairaq watukufu.. kuna vita kubwa nyingine mbele yenu, nayo ni (vita ya islahi), kupambana na kumaliza miongo mingi ya ufisadi na udhaifu wa idara za serikali. Marjaa Dini mkuu alisisitiza swala hili kupitia khutuba ya ushindi mioaka miwili iliyo pita, alisema kua: (Hakika vita hii –ambayo imechelewa sana- haitofautiani na vita ya kupambana na ugaidi kama sio zaidi, raia wa Iraq walio pigana dhidi ya magaidi wanaweza kushinda vita hii iwapo watakua na uongozi mzuri), kutumia njia za amani ndio sharti la kupana ushindi katika vita hii, jambo linalotia moyo asilimia kubwa ya waandamanaji wanajua umuhimu wa kuandamana kwa amani na kujiepusha na vitendo vya ukatili, vurugu mamoja na kuharibu mali za wananchi).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: