Marjaa Dini mkuu.. ukweli wa historia: Wananchi na taifa la Iraq vimemfanya asahau kujiombea mwenyewe.

Maoni katika picha
Mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ktika mkutano na waandishi wa habari, aliotangaza kufanikiwa kwa upasuaji wa Marjaa Dini mkuu na kuondoka Hospitalini amesema kua, kabla wakati na baada ya upasuaji Mheshimiwa alikua anaombea dua wananchi na taifa la Iraq wala hakujiombea yeye mwenyewe.

Sayyid Swafi akabainisha kua: “Jopo la madaktari limeeleza kwa ufupi kua Mheshimiwa Sayyid alikua anaongea nao, na kitu ambacho wamekibainisha sasa hivi na kitabaki kua historia kwenu ni kwamba Sayyid hakujiombea mwenyewe kabisa, hakusema ewe Mola niponye na unipe afya, alikua analiombea taifa la Iraq, amefanya hivyo kabla, wakati na baada ya upasuaji.

Wakati wote ulimi wake ulikua unaliombea taifa na raia wa Iraq, naamini kua ujumbe huu uko wazi kwa Iraq na watu wake, wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwapa neema ya kuwepo kwa Sayyid, mimi nilikua namhudumia nikamuambia: hakika kuwepo kwako ni miongoni mwa rehema za Mwenyezi Mungu kwetu, kama raia wa Iraq tuna deni kwako ewe bwana wetu, tunamuomba Mwenyezi Mungu atuonyesha Iraq yenye amani na utulivu, na wewe ushuhudie matunda ya nasaha na maelekezo yako unayo toa katika kipindi hiki”.

Dokta Ihsani Faraji mmoja wa madaktari walio mfanyia upasuaji amethibitisha kua muda wote wa upasuaji Sayyid alikua anaiombea Iraq na raia wake.

Nae Shekh Murtadha Hilliy mmoja wa wanafunzi wa Dini katika mji wa Najafu, amesema kua: “Hakika Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Sistani kuacha kujiombea yeye mwenyewe wakati huo wa hali ngumu na kuliombea taifa na raia wa Iraq sio jambo la kawaida, ni kilele cha juu kabisa cha kuwapenda watu na ukomavu wa Ikhlasi, maadili, ibada, Imani na roho, aidha ametupa ujumbe wa ulazima wa kulipa umuhimu taifa, kulilinda na kujitolea kwa ajili yake, ndio maana alitoa fatwa ya jihadi kifaya, amejitolea nafsi yake kwa ajili ya Iraq na raia wake. Ametoa maelekezo na nasaha wakati wote”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: