Kwa lugha mbalimbali: Yamewekwa mabango mengi ya kuelekeza mazuwaru.

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kurahisisha ufanyaji wa ziara kwa mazuwaru wote waarabu na wa ajemi, Atabatu Abbasiyya imesambaza mabango ya kuelekeza mazuwaru jirani na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, yanayo waelekeza mazuwaru sehemu tofauti wanazo hitaji kuzitembelea.

Mabango hayo yanaelekeza upande wa kibla pamoja na sehemu zingine, kama vile sehemu za kupumzika, vyoo, njia pamoja na kuelekeza mahala zilipo haram mbili tukufu.

Mabango yameandikwa katika zaidi ya lugha moja, yapo ya kiarabu, kifarisi na kiengereza, ili iwe rahisi kwa zaairu kutambua sehemu anayo taka kwenda pamoja na kuzipa kipaombele barabara zenye watu wengi.

Kumbuka kua kazi hii inatokana na mpango mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao unashughuli nyingi zinazo lenga kutoa huduma bora kwa mazuwaru, na kuwasaidia waweze kufanya ibada zao kwa urahisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: