Makubaliano ya kuongeza ushirikiano kati ya kikosi cha Abbasi na msaraba mwekundu.

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/ 26 Hashdi Shaábi) pamoja na kamati ya msalaba mwekundu, wamefanya makubaliano ya kuongeza ushirikiano katika kutoa huduma za kibinadamu kwa taifa la Iraq na raia wake.

Mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) Ustadh Maitham Zaidi amempokea ofisini kwake Ustadh Alaa Faham ambaye ni mwakilishi wa msalaba mwekundu katika mji wa Najafu pamoja na wajumbe wengine alio fuatana nao, wakajadili kwa pamoja namna ya kuongeza ushirikiano katika sekta ya kutoa huduma za kibinaadamu.

Kikao hicho pia kimejadili misaada ya kibinaadamu inayo tolewa moja kwa moja na kikosi cha Abbasi (a.s) sehemu mbalimbali, au kupitia vikundi vilivyo chini yake kama vile (Hamlatul-Wafaa) na idara za ustawi wa jamii zilizo chini yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: