Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu kinafanya mkutano na viongozi wa vitengo vya Ataba.

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kuboresha utendaji kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya mkutano na viongozi wa kitengo cha Ataba ndani ya ukumbi wa Imamu Qassim (a.s) siku ya Jumatano (26 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (22 Januari 2020m).

Mkutano huo umejadili mambo mbalimbali kuhusu maendeleo mapya na namna ya kunufaika na uzowefu walionao viongozi wa vitengo, baada ya kikao hicho kiongozi wa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu Dokta Muhammad Hassan Jaabir ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ya kukitumia kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu kufuatia umuhimu wa kuboresha utendaji, leo tumefanya mkutano pamoja na viongozi wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya kwa lengo la kuwaambia mambo tunayo kusudia kuyafanya siku za mbele chini ya mkakati tuliopanga, pamoja na kunufaika na uzowefu wao”.

Akaongeza kua: “Katika kikao hiki tumejadili nukta muhimu za kuboresha utendaji wetu, tunatarajia kikao hiki hakitakua cha mwisho, aidha kitakua kiunganishi baina yetu na vitengo vyote, yamefanyika mambo matatu ya msingi kwenye kikao hiki, ambayo ni: kuwasilisha mpango mkakati wa kitengo, kuwasilisha mapendekezo ya mpango kazi ndani ya taasisi husika na kuwasiliana na vitengo vingine katika kuboresha utendaji”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: