Muhimu na hivi punde.. msimamo wa Marjaa Dini mkuu kuhusu hali ya taifa kwa sasa.

Maoni katika picha
Mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa ya leo (28 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (24 Januari 2020m) ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amesoma nakala iliyo mfikia kutoka ofisi ya Marjaa Dini mkuu huko Najafu, inayo husu hali ya taifa kwa sasa.

Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amesema:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Mabwana na mabibi.. nakusomeeni kwa ufupi msimamo wa Marjaa Dini mkuu kuhusu hali ya taifa kwa sasa, kama ilivyo tufikia kutoka kwa Mheshimiwa Sayyid katika mji wa Najafu.

Kwanza: Hakika Marjaa Dini mkuu anasisitiza msimamo wake wa ulazima wa kuheshimu utawala wa Iraq na utulivu wa kisiasa pamoja na umoja wa taifa na raia, na kukanusha kila kinacho vunja heshima ya utaifa kwa namna yeyote, wananchi wanauhuru kamili wa kutumia njia za amani na kudai kila wanacho ona kinafaa katika taifa lao bila kuingiliwa na watu wa nje ya taifa.

Pili: Marjaa Dini anasisitiza umuhimu wa kufanya mabadiliko ya kweli ambayo raia wamekua wakiyadai kwa muda mrefu, na wamejitolea mno katika kudai mabadiliko hayo, hakika kuchelewa kutekeleza mabadiliko hayo hakusaidii lolote ispokua kurefusha muda wa kukosekana utulivu wa amani na siasa za taifa.

Tatu: Kuunda serikali mpya kumechukua muda mrefu tofauti na ule uliotajwa kwenye katiba, ni muhimu vikundi vyote visaidiane kumaliza tatizo hili chini ya misingi iliyopangwa, hakika ni hatua muhimu katika kumaliza matatizo yaliyopo.

Hakika Marjaa Dini mkuu anatoa wito kwa vikundi vyoto vya wairaq vitambue hatari inayo likumba taifa lao kwa sasa, wakubaliane kwa pamoja kumaliza hatari hiyo, waweke mbele maslahi ya taifa la Iraq ya sasa na baadae, na Mwenyezi Mungu ni mkuu wa kuwafikisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: