Mgahawa wa Swahibul-Juud: Tumegawa zaidi ya milo milioni tatu katika mwaka wa 2019m.

Maoni katika picha
Mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza kua jumla ya milo iliyogawa mwaka 2019m, ilifika milioni tatu na laki nne (3,400,000) kwa mazuwaru wa malalo takatifu na mingine tofauti na hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Aadil Hamami, amesema kua: “Mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ni mikono utoayo wema na ukarimu, imenyooshwa kukirimu wageni nayo ni alama ya ukarimu, uaminifu na kujitolea, hugawa chakula chenye baraka na tiba kwa mazuwaru wake na wa malalo ya ndugu yake Imamu Hussein (a.s), kama sehemu ya kukamilisha mwenendo na ukarimu alio onyesha katika vita ya Twafu, yeye ndiye mnyweshaji wenye kiu Karbala”.

Akasema kua: “Wanufaika wa chakula hicho ni:

Kwanza: Mazuwaru wa malalo tukufu, hupewa chakula katika ukumbi wa mgahawa uliopo ndani ya haram tukufu, au hupewa chakula kilicho wekwa kwenye vifungashio katika madirisha ya kugawia chakula ya nje.

Pili: Mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), mgahawa unanafasi kubwa ya kuandaa chakula cha mazuwaru, kuanzia zaairu wa kwanza hadi wa mwisho hasa wanaotoka nje ya Iraq.

Tatu: Wageni wa Atabatu Abbasiyya tukufu kutoka ndani na nje ya Iraq.

Nne: Waliofunga hupewa futari katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Tano: Waandamanaji walio weka kambi kwenye uwanja wa maandamano mjini Karbala.

Sita: Wafanya kazi wa kujitolea katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanao saidia kulinda amani na kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wakati wa ziara ya Ashura na Arubainiyya pamoja na ziara zingine zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.

Saba: Kwenye ziara maalum ambazo Atabatu Abbasiyya tukufu huenda kushiriki na kujenga hema makhsusi kwa ajili ya kugawa chakula kwa mazuwaru katika mji wa Samaraa, Kadhimiyya na Najafu”.

Akaongeza kua: “Vyakula hugawiwa vya aina mbalimbali kutokana na mapenzi ya mazuwaru, vilevile hupewa juisi, matunda na halawiyaat kulingana na wakati”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: