Waombolezaji wanamiminika katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Tangu siku ya Jumanne asubuhi waombolezaji wamekua wakimiminika katika malalo ya bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuomboleza kifo cha mbora wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s) katika aridh hii tukufu kwa mujibu wa riwaya ya tatu.

Asubuhi ya Jumanne makumi ya mawakibu za waombolezaji wameingia katika mji wa Karbala kuomboleza msiba huu, unao umiza roho ya kila muumini, sambamba na kumiminika maelfu ya mazuwaru kutoka mikoa tofauti ya Iraq wanaokuja kumpa pole mtoto wake Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kama kawaida Atabatu Abbasiyya tukufu imeweka utaratibu maalum katika kuomboleza msiba huu, imeandaa sehemu maalum ya kufanyia maombolezo sambamba na kuratibu matembezi ya mazuwaru na mawakibu, pamoja na kufanya majlisi tofauti za kuomboleza ndani ya haram tukufu.

Uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu unashuhudia na utaendelea kushuhudia kufanywa kwa majlisi nyingi za uombolezaji, mazingira yote yamejaa huzuni na majonzi, kuanzia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu hadi ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s).

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu ilikua imesha wekwa mapambo meusi yanayo ashiria msiba na mabango yaliyo andikwa mamne ya kuomboleza, kufuatia uchungu wanaopata waumini na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kutokana na msiba huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: