Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya apokea ujumbe wa muungano wa wanajeshi waliojeruhiwa na awahimiza kuendeleza ujemedari wao

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi jioni ya leo (5 Jamadal-Uula 1441h) sawa na (31 Januari 2020m), amepokea wajumbe wa muungano wa wanajeshi waliojeruhiwa, baada ya kumaliza kwao kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mheshimiwa amesisitiza kua Ataba tukufu ikopamoja nao, pia akawahimiza kuandika mambo waliyo fanya wakati wakipigana na magaidi wa Daesh, kwa lengo la kuyaingiza kwenye kitabu cha fatwa tukufu ya kujilinda kinacho andikwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kama sehemu ya kuenzi ushujaa wa wairaq katika kukomboa ardhi yao kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh.

Rais wa muungano wa wanajeshi waliojeruhiwa Ustadh Mikdad Rahim amesema kua: “Leo tumemzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na tumekutana na kiongzi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kumuambia baadhi ya matatizo na haki tunazonyimwa kama majeruhi, tumempa maelezo kuhusiana na muungano huu na kazi tunazo fanya katika kuhudumia wapiganaji wa Hashdi Shaábi waliojeruhiwa”.

Akaongeza kua: “Muungano huo unawanachama elfu (63) ambao ni askari wa jeshi la serikali na Hashdi Shaábi kutoka mikoa tofauti ya Iraq, lengo la muungano huo ni kuwahudumia askari wa Iraq waliojeruhiwa, sababu za kuanzishwa umoja huu ni kuwasaidia majeruhi wote bila ubaguzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: