Mafundi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wamemaliza kutengeneza dirisha la Swafi-Swafa na maandalizi ya kulibeba yanaendelea.

Maoni katika picha
Mafundi wa kutengeneza madirisha na milango ya kwenye makaburi matukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, wamemaliza kutengeneza dirisha la Athibu Alyamani ajulikae kama (Swafi-Swafa) –r.a- katika mkoa wa Najafu, maandalizi ya kulibeba kutoka Karbala na kuanza kulifunga yanaendelea.

Dirisha hilo litafungwa na mafundi walio litengeneza, linaingizwa kwenye orodha ya mafanikio yaliyo fikiwa, ikiwa ni pamoja na kutengenezwa kwa mihrabu ya Maqam ya kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) katika mazaru hiyo, iliyo tengenezwa na kufungwa mwaka jana.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naadhim Gharabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu wasifu wa dirisha hilo kua: “Dirisha limesanifiwa na kutengenezwa na kitengo chini ya watumishi wake, wamefanya kazi kwa umaridadi na umakini mkubwa kulingana na heshima na utukufu wa maqam hiyo, wamefanikiwa kulitengeneza vizuri sana na kulinda ubora wa (viwanda vya Iraq).

Akaongeza kua: “Dirisha lina urefu wa (mt 4.7) na upana wa (mt 3.60), kimo cha (mt 4.20), madini yaliyotumika ni dhahabu, fedha, silva na chuma, dhahabu iliyotumika inakaribia (kg 800) na fedha halisi (kg 220) na silva (tani 1) huku chuma kigumu kikiwa (tani 3.5), na karibu (kg 50) za mina iliyo tumika kuweka nakshi kwenye maandishi”.

Akabainisha kua: “Mbao za Burumi ndio zimetumika katika kutengeneza umbo la dirisha, mbao hizo zinasifa nyingi, zina uwezo mkubwa wa kuvumilia mazingira na kubeba mizigo mizito, haziliwi na mchwa au mdudu yeyote, mbao hizo ndio zimetengenezewa umbo la dirisha na nakshi za ndani”.

Kumbuka kua kazi hii imefanywa baada ya kusainiwa mkataba kati ya uongozi mkuu wa mazaru za kishia na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, kufuatia uwezo na uzowefu wa watumishi wake katika kutengeneza madirisha hayo, na sasa wanaweza kufanya hadi kazi za nje ambazo kwa kiwango kikubwa zimechangia kuongeza uwezo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: