Marjaa Dini mkuu amelaani uvunjifu wa amani uliotokea katika mji wa Najafu na amesisitiza ulazima wa jeshi la serikali kubeba jukumu lake.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amelaani uvunjifu wa amani uliotokea Jumatano iliyopita katika mji wa Najafu, na ametoa pole kwa familia zilizo poteza wapenzi wao pamoja na kuwaombea majeruhi wapone haraka, amesisitiza ulazima wa jeshi la serikali kubeba jukumu la kulinda amani na utulivu, wala hakuna sababu za kutofanya hivyo.

Amesema hayo katika khutuba ya swala ya Ijumaa leo (12 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (7 Februari 2020m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hussein (a.s) iliyo tolewa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.

Lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

(Wakati ambao Marjaa Dini anakemea uvunjifu wa amani wa kila aina, na kuzipa pole familia zilizo poteza wapenzi wao na kuwaombea majeruhi wapone haraka, anasisitiza aliyosema siku za nyuma kua hatuwezi kuacha kutegemea jeshi la serikali katika kuzuwia fujo na vurugu na kujitenga na serikali kwa ujumla, jeshi ndio lenye jukumu la kulinda amani na utulivu, pamoja na kuimarisha amani na utulivu kwenye viwanja vinavyo tumiwa na waandamanaji, waovu wanajipenyeza na kufanya uharibifu jambo hilo halikubaliki, kazi ya kuwazuwia waovu hao ni jukumu la jeshi, wanatakiwa walifanye kwa weledi mkubwa bila kuleta madhara kwa watu wanaofanya maandamano ya amani, pamoja na kuzuwia uharibifu wa mali za umma na binafsi kwa aina yeyote ile).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: