Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s).
Hafla imefanywa katika ukumbi wa mlango wa Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu Dokta Afdhalu Shami na baadhi ya viongozi wa kidini na kisekula, pamoja na kundi kubwa la zuwaru waliokuja kuadhimisha tukio hili tukufu.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ukafuata ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya uliowasilishwa na Shekhe Ali Mujaan, ameanza kwa kutoa pongezi kwa wahudhuriaji na umma wa kiislamu kwa kuadhimisha mazazi ya wakweli wawili (a.s), akaeleza hatua za maisha yao sambamba na changamoto walizopata.
Mjumbe wa kamati ya maulidi katika Ataba tukufu Sayyid Aqiil Yasiri amesema: “Hafla ilikuwa na vipengele mbalimbali, miongoni mwake ni: usomaji wa qaswida, mashairi na tenzi maalum kuhusu tukio hili takatifu”.
Akaongeza kuwa “Hafla imehitimishwa kwa kuwapa zawadi washindi wa shindano la kitamaduni lililosimamiwa na uongozi mkuu wa Ataba tukufu, kupitia kitengo cha habari na utamaduni, kulikuwa na washiriki zaidi ya 4500, huku 3600 wakitoa majibu sahihi jambo lililopelekea kupiga kura ili kupata washindi kumi wanaotakiwa kupewa zawadi”.
Atabatu Abbasiyya hufanya program maalum katika kuadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) kwa lengo la kuimarisha mafundisho ya kidini kwa zuwaru.



















