Kituo hicho ni sehemu ya upanuzi wa Darul-Hayaat kwenye mji tajwa, inayo tumika kupokea watu walio ambukizwa virusi vya Korona, kituo kina:
- - Vyumba (56) kila chuma kina ukubwa wa (2m12).
- - Vyumba (3) vya wahudumu wa afya kila chumba kina ukubwa wa (2m24).
- - Chumba cha kubadilishia nguo wahudumu wa afya chenye ukubwa wa (2m6).
- - Chumba cha kuwekea vifaa kinaukubwa wa (2m6).
- - Sehemu ya mapokezi na ukumbi mkubwa wa wazi wenye ukubwa wa (2m1550).
Kumbuka kua mradi huu ni sehemu ya kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia sekta ya afya, aidha ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kulinda jamii na virusi vya Korona, ndipo mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wakaanza kazi ya ujenzi wa kituo hiki kwa kufuata maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, katika mji wa Imamu Hussein (a.s) hapa Karbala, na kusimamiwa na idara ya madaktari wa Ataba na hospitali ya rufaa Alkafeel.