Atabatu Abbasiyya tukufu inazindua kituo cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona katika mkoa mtukufu wa Karbala

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu leo siku ya Jumamosi asubuhi mwezi (17 Shabani 1441h) sawa na (11 Aprili 2020m) imezindua kituo cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Imamu Hussein (a.s) hapa Karbala, kiitwacha (Jengo la Alhayaat la pili), baada ya mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi kukamilisha ujenzi wa mradi huo kwa mudu mfupi usio zidi siku kumi na tano.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wakiongozwa na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar na jopo la wajumbe wa idara yake, pamoja na mkuu wa mkoa wa Karbala na mkuu wa idara ya afya.

Kituo hicho ni sehemu ya upanuzi wa Darul-Hayaat iliyokuwa ikitumika kupokea watu walio ambukizwa virusi vya Korona. Kituo kina:

  • - Vyumba (56) kila chuma kina ukubwa wa (2m12).
  • - Vyumba (3) vya wahudumu wa afya kila chumba kina ukubwa wa (2m24).
  • - Chumba cha kubadilishia nguo wahudumu wa afya chenye ukubwa wa (2m6).
  • - Chumba cha kuwekea vifaa kinaukubwa wa (2m6).
  • - Sehemu ya mapokezi na ukumbi wa wazi wenye ukubwa wa (2m1550).

Kumbuka kua mradi huu ni zawadi kutoka hospitali ya rufaa Alkafeel na umetekelezwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, pia ni sehemu ya kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia sekta ya afya na sehemu ya mkakati wa Ataba wa kulinda jamii dhidi ya virusi vya Korona, aidha ni maelekezo ya moja wa moja kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, aliyetaka tujenge kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Imamu Hussein (a.s) hapa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: