Maswali kuhusu zakatul-fitri

Maoni katika picha
Lini huwajibika zakatul-fitri?

Wakati gani unatakiwa kutoa zakatul-fitri?

Ni upi wakati bora wa kutoa zakatul-fitri?

Je inafaa kuchelewa kutoa zakatul-fitri?

Je inafaa kuacha kutoa zakatul-fitri na kuitoa wakati mwingine?

Wakati gani hutakiwi kutoa zakatul-fitri?

Maswali hayo na mengine mengi yamejibiwa na Sayyid Muhammad Mussawi kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, kwa mujibu wa fatwa za marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani na kurushwa kwenye mitandao ya kijamii ambayo ipo chini ya Ataba pamoja na toghuti ya kimataifa ya Alkafeel.

Kumbuka kuwa kiwango cha pesa ya zakatul-fitri mwaka huu ni (1500) dinari za kiiraq kwa mtu mmoja, badala ya unga (kwa kiwango cha chini).

Kiwango cha lazima kisheria ni pishi, pishi moja ni sawa na (kilo 3) za ngano (unga), shairi, zabibu, mchele, tende au nafaka yeyote inayopendwa na watu wa mji husika, au utalipa pesa inayo lingana thamani na vitu hivyo, ni wazi kuwa thamani ya vitu hivyo inatofautiana kutokana na kutofautiana kwa nchi na maeneo, hivyo unatakiwa kuangalia thamani ya kilo katika mji wako kabla ya kutoa hela za zakatul-fitri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: