Eneo la katikati ya haram mbili takatifu linashuhudia opresheni kubwa ya kupuliza dawa

Maoni katika picha
Eneo la katikati ya haram mbili tukufu linashuhudia opresheni kubwa ya kupuliza dawa kwenye uwanja wa katikati na sehemu iliyo pauliwa pamoja na sehemu yote iliyo tandikwa mazulia, chini ya mkakati wa kujilinda na virusi vya Korona, ili kuhakikisha usalama wa mazuwaru na watumishi, shughuli hiyo inafanywa wakati ambao kuna mazuwaru wachache kutokana na marufuku ta kutembea iliyo wekwa katika mkoa huu.

Haya yamesemwa na raisi wa kitengo cha kusimamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu alipo ongea na mtandao wa Alkafeel, akasema kuwa: “Kazi hii ni sehemu ya opresheni kubwa iliyo anza tangu siku za kwanza za kutokea kwa janga hili, imekua ikiendeshwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi kupitia kamati ya kupambana na maambukizi katika Atabatu Abbasiyya”.

Akaongeza kuwa: “Opresheni hii imehusisha sehemu ya nje katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na uwanja wa katikati ya haram mbili hadi sehemu iliyo pauliwa na sehemu zilizo wekwa mazulia”.

Akafafanua kuwa: “Kikosi kilicho endesha opresheni hiyo kimetumia vifaa vilivyo tengenezwa na shirika la Khairul-Juud vyenye ubora mkubwa”.

Mwishini mwa maelezo yake akasema: “Kutokana na maelekezo yaliyo tolewa na idara ya afya katika Atabatu Abbasiyya, tumechukua hatua zote za kuwakinga watumishi wetu na maambukizi, tumepunguza idadi ya wafanyakazi katika kila zamu, pamoja na kuwapulizia dawa za kuuwa bakteria na virusi kila wanapo maliza kufanya kazi”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua hatua mbalimbali za kujikinga na maambukizi ya virusi kvya Korona, na inafanyia kazi maelekezo yanayo tolewa na idara ya afya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: