Madaktari wa hospitali ya Alkafeel wamefanikiwa kumtibu mgonjwa wa kudhoofika kwa viungo mwenye umri wa miaka thelathini

Maoni katika picha
Jopo la madaktari bingwa wa upasuaji katika hospitali ya rufaa Alkafeel wamefanikiwa kumtibu mgonjwa mwenye umri wa miaka thelathini aliyekuwa na tatizo la kudhoofika kwa viungo vyake baada ya kufanyiwa ubasuaji.

Dokta Khalid Siraji amesema: Jopo la madaktari limefanikiwa kufanya upasuaji na upandikizaji wa chembechembe hai.

Akabainisha kuwa: mgonjwa alikuwa na tatizo la kudhoofika kwa viungo na uzito wa utambuzi.

Akafafanua: Hospitali ya Alkafeel inamaabara ya kisasa yenye vifaa tiba bora, ndio vilivyo tuhamasisha kufanya upasuaji ambao ulikuwa sio rahisi kufanywa ndani ya Iraq siku za nyuma.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inafanya kila iwezalo kutoa huduma bora kwa vifaa-tiba vya kisasa inavyo miliki chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambolo limeifanya kutoa ushindani mkubwa katika hospitali kubwa za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel kila baada ya muda Fulani hualika madaktari bingwa wa maradhi tofauti sambamba na kupokea wagonjwa wa maradhi mbalimbali ambayo wapo katika hatua tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: