Kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel kimetengeneza masafa maalum ya kurusha matangazo ya matembezi ya wapenzi wa Hussein

Maoni katika picha
Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel kimetengeneza masafa maalum ya kurusha matangazo kwa ubora mkubwa (clean), ya matembezi ya wapenzi wa Imamu Hussein (a.s), kuanzia sehemu za mbali kabisa kusini mwa Iraq hadi kwenye kaaba ya msimamo Karbala tukufu, kupitia mitambo ya kisasa inayo endeshwa na watu wenye ujuzi mkubwa kwenye sekta hiyo, na kuhakikisha ziara hiyo inashuhudiwa kila sehemu duniani.

Makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Ahmadi Swadiq amesema: “Hakika ni sehemu ya mkakati uliowekwa na uongozi wa kitengo kulingana na mazingira tunayoishi kwa sasa kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya Korona, tunatoa wito kwa vyombo vyote vya habari vya kitaifa na kimataifa vinavyo penda kurusha matangazo ya ziara hii vitumie anuani zifuatazo:

Satellite: Eutelsat 7A at 7.0 East(W3A
DOWNLINK:12680.200 H
MOD:DVBS2
QPSK
FEC:5/6
Sr :3250
HD/MPEG-4
Pia tumetengeneza link ambayo utapata matangazo hayo yakiwa na ubora mkubwa, https://www.youtube.com/channel/UCaaBs5EwkPCs1wXIeMPP0bA”.

Akasema: “Masafa hiyo hairushi matembezi ya Arubaini peke yake, bali inarusha harakati mbalimbali zinazo fanywa ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya hadi siku ya ziara, mwezi ishirini Safar”.

Kumbuka kuwa kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel kinafanya vizuri sana katika matangazo yake, watumishi wake wanaujuzi mkubwa unao wafanya wakubalike na vyombo vyote vya habari, hivyo habari zao zinarushwa na makumi ya luninga za ndani na nje ya Iraq.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba: (+9647706054144 / +9647732407567 / +9647805085858).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: