Kwa Karkha yake na Raswafa yake: Maukibu (823) zimetoa huduma katika ziara ya Arubaini mkoani Bagdad

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu imesema kuwa, idadi ya maukibu zilizo hudumia mazuwaru wa Arubaini katika mkoa wa Bagdad pamoja na zile za Karkha na Raswafa mwaka huu imefika (8475) zilizo sajiliwa rasmi, bado kuna makumi ya Husseiniyya, nyumba za watu na maukibu ambazo zimetoa huduma tangu siku ya kwanza bila kusajiliwa, maukibu zote hizo zimetoa huduma ndani ya eneo la mkoa wa Bagdad.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan, akaongeza kuwa: “Mkoa wa Bagdad ni moja ya sehemu ambazo mazuwaru wa Arubaini hupita, hususan wanaotoka mkoa wa Mosul, Karkuuk, Swalahu-Dini, Diyala pamoja na mazuwaru wa mkoa huo (Bagdad), mawakibu hizo zimeweka kambi kwenye barabara zote zinazo tumiwa na mazuwaru, huku barabara zinazo tumiwa na mazuwaru wengi zikipewa kipaombele zaidi”.

Akafafanua: “Kuna maukibu (2829) zinashirikiana na maukibu za mikoa mingine kutoa huduma katika mkoa wa Karbala na kwenye barabara zinazo elekea huko, hasa barabara ya (Bagdad – Karbala)”.

Akaongeza kuwa: “Maukibu hizo hazijaishia kutuo huduma ya chakula na vinywaji peke yake, bali wametoa pia huduma za afya kufuatia kuwepo kwa janga la virusi vya Korona, sambamba na mchango wao katika kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, baada ya misafara ya mazuwaru kuisha katika mkoa huu, wahudumu wa maukibu wataenda Karbala kufanya ziara na kupata utukufu mara mbili: wa kutoa huduma kwa mazuwaru na kufanya ziara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: