Kutokana na huzuni ya kumbukumbu ya kifo cha mzazi wake Ataba imewekwa mapambo meusi

Maoni katika picha
Mazingira ya huzuni yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na kukumbuka kifo cha bibi mtakatifu Ummul-Banina mama wa Abulfadhil Abbasi na ndugu zake (a.s), ambaye tarehe ya kifo chake inasadifu kesho siku ya Jumatano mwezi (13 Jamadal-Aakhar 1442h) sawa na tarehe (27 Januari 2021m), kutakuwa na ratiba ya uombolezaji na utoaji wa huduma kwa ajili ya kuomboleza msiba huo uliotokea katika nyumba ya Utume mwaka (64) hijiriyya, wafuasi na wapenzi wao huomboleza msiba huo kila sehemu ya dunia.

Atabatu Abbasiyya tukufu na korido zake imewekwa mapambo meusi, na juu ya kuta zake yamewekwa mabango yenye ujumbe unao onyesha msiba na huzuni pamoja na heshima kubwa ya bibi huyo mtukufu (a.s).

Kama ilivyo kawaida katika kuomboleza tarehe za vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum kufuatia tukio hilo chungu.

Kumbuka kuwa mwezi kumi na tatu Jamadal-Aakhar mwaka wa (64h) mama mtukufu Ummul-Banina mke wa kiongozi wa waumini (a.s), Fatuma bint Hizam Alkilabiyya Al-Aamiriyya, aliyepewa jina la Ummul-Banina kwa sababu alikua na watoto wa kiume wanne wote waliuwawa katika vita ya Twafu huko Karbala kwa ajili ya kumnusuru bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), alifia Madina na kuzikwa katika makaburi ya Baqii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: