Hospitali ya rufaa Alkafeel imefanikiwa kwa asilimia (%95) katika upasuaji wa moyo kwa watoto.

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya upasuaji (600) wa moyo kwa watoto na kupata mafanikio ya asilimia (%95), aidha imesema kuwa inamiliki kituo cha kisasa cha upasuaji wa moyo, chenye uwezo wa kufanya upasuaji hadi kwa mtoto mwenye umri wa chini ya miezi mitatu (3).

Mkuu wa hospitali Dokta Jaasim Ibrahimi amesema kuwa: “Ndani ya miaka minne tumefanya upasuaji wa moyo (600) kwa watoto wenye umri tofauti, kiwango cha mafanikio ni asilimia (%95), kiwango hicho kinachuana na vituo vikubwa vya upasuaji wa moyo kwa watoto duniani”.

Akataja sababu ya mafanikio hayo ni vifaa-tiba vya kisasa walivyo navyo na madaktari bingwa pamoja na wauguzi mahiri wanao endana na maendeleo ya kitabibu duniani.

Mkuu wa kitengo cha upasuaji wa moyo kwa watoto Dokta Ahmadi Abudi amesema kuwa: “Kituo hiki pamoja na uchanga wake kinatoa ushindani mkubwa kwa vituo vya upasuaji wa moyo vilivyo endelea katika nchi zingine”.

Akasema kuwa: “Kituo kilianzishwa mwaka (2017m) ndani ya hospitali, kina jengo la chini na vifaa-tiba vyenye ubora mkubwa pamoja na watumishi walio bobea, kimekua mbadala muafaka kwa wagonjwa waliokua wanalazimika kwenda nje ya nchi kutafuta matibabu”.

Akaongeza kuwa: “Kazi ilianza kuongezeka tangu kufunguliwa kwake hadi mwezi Oktoba mwaka (2020m) tukawa tumesha fanya jumla ya upasuaji (600), huku upasuaji (300) ukiwa umefanya na madaktari wa kiiraq na (300) ukifanywa na jopo la madaktari wa kigeni”.

Akafafanua kuwa: “Kiwango cha mafanikio ya upasuaji wa tumbo kimefanikiwa kwa asilimia (%97) na upasuaji wa moyo tumefanikiwa kwa asilimia (%94) nacho ni kiwango kinacho chuana na vituo vikubwa vya moyo duniani”.

Daktari bingwa wa moyo kwa watoto akasema: “Jambo kubwa lililopo katika kituo hiki ni uwezo wake wa kufanya upasuaji kwa watoto wadogo na wenye kilo chache, wenye matatizo ya moyo”.

Kiongozi wa kituo cha upasuaji wa moyo katika hospitali hiyo, Dokta Ahmadi Ali Almayahi amesema kuwa: “Kituo hiki kinavifaa-tiba vya kisasa sawa na vile vilivyopo katika hospitali kubwa za kimataifa” akabainisha kuwa: “Mgonjwa huwa chini ya uangalizi mkubwa katika kipindi chote anachokua hospitalini”.

Almayahi akasema: “Madaktari na wauguzi waliopo katika kituo hiki wanamafunzo maalum ya kuhudumu kwenye vituo vya aina hii, wana uzowefu mkubwa wa kuhudumia mtu aliye fanyiwa upasuaji wa moyo sawa awe mdogo au mkubwa”.

Akasema: “Kituo kinaweza kutoa huduma hadi kwa watoto wenye uzito chini ya (kilo 5) na umri chini ya miezi (3)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: