Maahadi ya Quráni tukufu inashiriki katika vikao vya usomaji wa Quráni mkoani Baabil

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia tawi la mkoa wa Baabil, ndani ya mazaru ya Zaidu Shahidi (a.s) kwa kushirikiana na uongozi wa mazaru hiyo pamoja na kituo cha maarifa ya Quráni.

Sayyid Muntadhir Mashaikhi kiongozi wa tawi la Maahadi katika mkoa wa Baabil amesema: “Kisomo hiki kilianza toka siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ni moja ya harakati zinazo fanywa na Maahadi na matawi yake mikoani, mwaka huu imefanywa katika mazaru ya Zaidu Shahidi (a.s), nao ni mkusanyiko mkubwa zaidi wa usomaji wa Quráni, unaofanywa kwa kuzingatia kanuni zote za kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona, pamoja na mambo mengine”.

Akaongeza kuwa: “Kisomo kiliandaliwa mapema pamoja na kuweka mahitaji yote muhimu, kama vile jukwaa na sehemu ya kukaa wasomaji na misahafu. Wasomaji wengi wa Quráni tukufu wameshiriki baada ya kupewa mualiko mapema”.

Akabainisha kuwa: “Usomaji unaanza saa kumi na moja Alasiri, kila siku husomwa juzuu moja kwa mzunguko wa wasomaji watano, amboa hutumia muda wa saa moja, kisomo hiki kitaendelea hadi mwisho wa mwezi huu mtukufu”.

Kumbuka kuwa matawi ya Maahadi ya Quráni katika mji wa Karbala na mikoani, yanatekeleza ratiba baalum ya usomaji wa Quráni ndani ya mwezi wa Ramadhani katika Husseiniyya na Mazaru mbalimbali, pamoja na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: