Kongamano litaangalia maendeleo yaliyopatikana katika sekta ya udaktari katika miaka ya hivi karibuni, sambamba na maendeleo ya kimaabara, maendeleo hayo yamewezesha kufanyika tafiti muhimu, ambazo zimesaidia kuboresha matibabu kwa kiwango kikubwa, mazingira yameruhusu chuo kikuu cha Al-Ameed kufanya kongamalo la awamu ya pili la kitabibu, ili kuendana na maendeleo hayo pamoja na kuendeleza tafiti za kielimu katika kipindi ambacho zinahitajika zaidi kwa ajili ya kupambana na janga la virusi vya Korona pamoja na magonjwa mengine.
Link ya kujisajili kwenye kongamano ni: black_small_square na mtandao maalum ni: https://conference.alameed.edu.iq/
Mada zitakazo wasilishwa kwenye kongamano hilo ni:
- - Maendeleo ya kielimu katika sekta ya utabibu na uhandisi.
- - Matibabu ya moyo kwa ndani.
- - Janga la Korona na changamoto zake nchini Iraq.
- - Maradhi ya damu.
- - Afya ya uzazi.
- - Uzuri wa tiba ya meno.
- - Uuguzi wa kitanda na matibabu.
- - Utengenezaji wa dawa.
- - Mtazamo mpya katika huduma za afya na mafunzo ya uuguzi.
Tambua kuwa chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya juhudi ya kuboresha tafiti za kielimu katika sekta ya utabibu, pamoja na kusaidia kuelimisha jamii mambo ya afya, sambamba na kuweka mazingira wezeshi ya kufanya tafiti mbalimbali za kitabibu.