Kikosi cha Abbasi kimeratibu warsha ya kielimu kwa watumishi wa afya wa Karkuuk

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) kinafanya warsha kuhusu program za kusimamia mitambo ya mawasiliano kwa watumishi wa idara ya afya ya Karkuuk.

Kiongozi wa mawasiliano katika kikosi cha Abbasi kwenye mji wa Bashiri bwana Karaar Bashiri amesema kua: “Warsha hiyo imefanywa kufuatia maombi ya idara ya afya ya Karkuuk na maelekezo ya uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Walengwa wa warsha hiyo ni watumishi wa afya wanaofanya kazi katika vituo vilivyopo mjini hapo”.

Idara ya afya ya Karkuuk imekishukuru kikosi cha Abbasi kwa kuwasaidia bila kuchoka katika mambo mbalimbali.

Kumbuka kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) kinaendelea kusaidia idara na taasisi za serikali kwenye mikoa tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: