Kidini.. kitamaduni.. kiutumishi: Shughuli za maukibu ya Ashbaalu-Twafu zinaendelea

Maoni katika picha
Idara ya Habari chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeunda maukibu iitwayo (Ashbaalu-Twafu), imeanza kutoa huduma tangu siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Muharam 1443h.

Maukibu hii ni maalum kwa watoto wenye umri wa miaka (7 – 12), wao ndio wajumbe wa maukibu hiyo na watoa huduma, kila kitu kwenye maukibu hiyo kipo chini ya usimamizi wao, wanasimamiwa na viongozwa wa idara tajwa.

Maukibu hiyo ipo katika barabara ya Baabu-Bagdad, karibu na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), inatoa huduma za kitamaduni na kidini, kwa mfano kufanya majaalis za matam na majaalis za mashairi, ufundishaji wa hati na uchoraji, sambamba na kuwepo maktaba katika maukibu, yenye majarida mengi ya Husseiniyya yanayo endana na rika la umri wao, yaliyo chapishwa na idara ya watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Rais wa kitengo hicho Shekh Ammaar Hilali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Huu ni mwaka wa kwanza wa maukibu hii tuliyo ipa jina la (Maukibu Ashbaalu-Twafu), kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu na baraka za Imamu Hussein (a.s) itafikia lengo kusudiwa, tunatarajia miaka ijayo iweze kuwa mfano bora katika utoaji wa huduma za Husseiniyya”.

Akaongeza kuwa: “Tulikua na ham kubwa ya kutengeneza maukibu ya aina hii, tulihisi umuhimu huo kutokana na kutokuwepo kwa maukibu kama hii katika uwanja wa kutoa huduma, tumefungua mlango wa kheri kwa watu wengine pia, wataanzisha mawakibu kama hii, ambayo kwa kweli ni shule ya bure katika maswala ya Husseiniyya”.

Kumbuka kuwa jambo kubwa katika maukibu hii inatoa huduma tofauti kwa wakati mmoja, wanufaika wa kwanza ni Watoto wanaotoa huduma, kwani wanapata malezi sahihi, na kuwaandaa katika maswala ya Husseiniyya, na wanafundishwa namna ya kuamiliana na swala hili, sambamba na kuwaandaa kinafsi namna ya kuamiliana na jamii kwa ujumla, aidha wanazowea mazingira ya mwezi wa Muharam, bila kusahau maukibu inatoa huduma nyingi kwa mazuwaru, miongoni mwa huduma hizo ni: ugawaji wa maji, matunda, vinywaji, na mengineyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: