Hili kaburi la Hussein (a.s) aliyeuawa ugenini akiwa na kiu

Maoni katika picha
Imekuja katika uhakiki wa Sayyid Muqarram: Wakati Imamu Sajjaad (a.s) alipoenda alikuta watu wa kabila la bani Asadi wakiwa wamekusanyika mbele ya maiti, wametahayali hawajui la kufanya, hawatambua maiti hizo kwani zilikua hazina vichwa, wakawa hawajui hizo maiti ni za kinanani, kutoka familia gani, akaanza kuwaelekeza (a.s) miili ya maiti hizo takatifu, akawatajia majina yao, akawaonyesha maiti za bani Hashim na maiti za wafuasi wao, wakalia sana.

Kisha Imamu Zainul-Aabidina (a.s) akaenda kwenye muili wa baba yake, akasimama na kulia, akaenda hadi sehemu ya kaburi, akatoa udongo kidogo mara akakuta kaburi limeshajimbwa, akamshika mgongoni huku anasema “Bismilahi wa fii sabili Llahi wa alaa milati Rasulu-Llahi, swadaqa LLahu wa Rasuuluhu maashaa-Allahu laa quwwata illa billahil-aliyyul-adhim”.

Akamshusha kaburini peke yake bila kusaidiwa na bani Asadi, akawaambia: “Hakika ninaye anaenisaidia”.

Alipomlaza katika mwanandani, aliweka shavu lake kwenye pua yake takatifu kisha akasema: “Imefaulu ardhi iliyobeba muili wako mtukufu, hakika dunia baada yako inagiza na akhera kwa nuru yako inamwanga, usiku hatupati usingizi, tunahuzuni muda wote, hadi Allah atakapo mchagulia mtu wa nyumbani kwako nyumba sawa na yako, amani iwe juu yako ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na rehema zake na baraka zake”.

Akaandika juu ya kaburi: “Hili kaburi la Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s) aliyeuawa ugenini akiwa na kiu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: