Nyakati na ratiba ya mawakibu za (zanjiil) katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika taifa la Iraq na ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimeandaa ratiba maalum ya mawakibu Husseiniyya za (zanjiil) zitakazo shiriki katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) mwaka huu 1443h.

Rais wa kitengo bwana Riyadhu Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tunatarajia viongozi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya kutoka mikoa yote ya Iraq wafuate ratiba, tambua kuwa ratiba hii inaanzia muda wa kuondoka kwenye jukwaa lililopo karibu na barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s) hadi kuingia katika Atabatu Husseiniyya tukufu kisha kuelekea katika Atabatu Abbasiyya na kumaliza matembezi yao hapo”.

Salmaan amezitaka mawakibu kuzingatia yafuatayo: “Kutohalifu utaratibu uliopangwa kwa ajili ya kumhudumia Imamu Hussein (a.s) na mazuwaru wake, sambamba na kutekeleza kanuni za kujikinga na maambukizi kwa kufanyia kazi maelekezo ya idara ya afya, kila maukibu itapewa nafasi mbili, nafasi ya (zanjiil) na nyingine ya (matam), zitaomboleza kwa mpangilio wa mikoa kama itakavyo tangazwa, kiongozi wa maukibu atagonga muhuri kila maukibu yake inapo shiriki”.

Ratiba ipo kama ifuatavyo:

Jeduali la ratiba

15 na 16 Safar 1443 hijiriyya

Kuwasiri kwa mawakibu kutoka mikoa yote.

16 Safar 1443 hijiriyya.

  • 1- Mkoa wa Dhiqaar na wilaya zake na vitongoji vyake kuanzia saa 1 hadi saa 3 asubuhi.
  • 2- Mkoa wa Bagdad wilaya zake na vitongoji vyake kuanzia saa 3 hadi saa 5 asubuhi.
  • 3- Mkoa wa Najafu wilaya zake na vitongoji vyake kuanzia saa 7 hadi saa 8 baada ya Adhuhuri.
  • 4- Mkoa wa Diwaniyya wilaya zake na vitongoji vyake kuanzia saa 8 hadi ya 10 Alasiri.
  • 5- Kadhimiyya takatifu kuanzia saa 10 hadi saa 12 jioni.
  • 6- Mkoa wa Misaan kuanzia saa 1 hadi saa 3 usiku.
  • 7- Mkoa wa Diyala kuanzia saa 3 hadi saa 5 usiku.
  • 8- Nchi za kiarabu na kiislamu kuanzia saa 5 hadi saa 7 usiku.

17 Safar 1443h

  • 1- Mkoa wa Basra wilaya zake na vitongoji vyake kuanzia saa 1 hadi saa 3 asubuhi.
  • 2- Mkoa wa Baabil wilaya zake na vitongoji vyake kuanzia saa 3 hadi saa 5 asubuhi.
  • 3- Mkoa wa Waasit wilaya zake na vitongoji vyake kuanzia saa 7 hadi saa 9 Alasiri.
  • 4- Mkoa wa Karkuuk na Nainawa wilaya yake na vitongoji vyake kuanzia saa 9 hadi saa 11 jioni.
  • 5- Mkoa wa Muthanna wilaya zake na vitongoji vyake kuanzia saa 1 hadi saa 3 usiku.
  • 6- Mkoa wa Swalahu-Dini wilaya zake na vitongoji vyake kuanzia saa 3 hadi saa 5 usiku.
  • 7- Nchi za kiarabu na kiislamu kuanzia saa 6 hadi saa 7 usiku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: