Kwa upasuaji wa aina yake.. kupandikiza ute bandia kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka arubaini

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, limefanya upasuaji na kupandikiza ute wa kwenye maungio ya mifupa kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka arubaini.

Daktari pingwa wa mifupa katika hospitali hiyo Dokta Khalidi Siraji amesema kuwa: “Mgonjwa alikua na tatizo la kukauka ute wa kwenye maungio ya mifupa, madaktari wamefanya upasuaji na kumuwekea ute wa kutengenezwa”, akaongeza kuwa: “Upasuaji umefanikiwa na mgonjwa anaendelea vizuri”.

Siraji akasema: “Vifaa-tiba vya kisasa vilivyopo katika hospitali ya rufaa Alkafeel, ambavyo ni sawa na vile vilivyopo katika hospitali kubwa za kimataifa, ni msaada mkubwa wa kufanya matibabu ya aina hii”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hutoa huduma bora daima kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeifanya kuwa sawa na hospitali kubwa za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alakafeel hualika madaktari bingwa wa fani tofauti kila baada ya muda, sambamba na kupokea wagonjwa walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: