Kuendeleza mafanikio ya kitabibu katika hospitali ya Alkafeel upande wa upasuaji wa macho

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel mjini Karbala, limetangaza kufanikiwa kurudisha uoni kwa mtoto aliyekuwa ameupoteza, wamesema kuwa wanaendelea kupata mafanikio hayo kutokana na kuwepo kwa vifaa-tiba vyote vya lazima.

Daktari bingwa wa macho katika hospitali hiyo, Dokta Salaam Qar’awi amesema kuwa: “Jopo la madaktari limefanikiwa kumfanyia upasuaji wa macho mtoto mwenye umri wa miaka (10), pamoja na kuondoa alama nyeusi na kupandikiza mboni tambuzi (trifocal IOL) kwenye macho yake”, akafafanua kuwa “Upasuaji umefanywa kwa uangalifu na weledi mkubwa”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya matibabu hayo, mtoto ameweza kuona vizuri masafa marefu na mafupi bila kutumia miwani”, akasema: “Upasuaji ulitumia takika (10) tu”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inatoa huduma bora daima kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa chini ya madaktari bingwa na wauguzi mahiri kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa katika hospitali za kimataifa duniani.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa kila wakati, sambamba na kupokea wagonjwa walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: