Kutoa wahitimu 586 wanawake katika uhadhiri wa Husseiniyya

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mbora wa wanawake (a.s), idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imetoa wahitimu (586) wanawake wahadhiri wa Husseiniyya, kama sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Zaharaa (a.s), asubuhi ya Jumatatu mwezi (20 Jamadal-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (24 Januari 2022m) katika ukumbi wa kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s) katika mji wa Karbala chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na wimbo wa taifa sanjari na wimbo wa Lahnul-Ibaa, halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wetu watukufu, baada ya hapo makamo kiongozi mkuu wa idara bibi Taghridi Tamimi akaongea kuhusu tukio hilo, akaanza kwa kupongeza washiriki kutokana na tukio hilo tukufu, akasisitiza ulazima wa kushikamana na mwenendo wa bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na kuifasiri historia yake kwa vitendo, miongoni mwa kuelekea utekelezaji wa hilo ni hii hafla tukufu ya Fatwimiyya, akafafanua kuwa: “Mradi wa wahadhiri wa kike wa Husseiniyya unapewa umuhimu mkubwa, na umekua ukipata muitikio mkubwa mwaka baada ya mwaka”.

Akaendelea kusema: “Kundi hili ni moja kati ya makundi matatu ya wahitimu, wanafunzi waliohitimu mwaka 2018 ambao ndio kundi la kwanza la mradi huu walikua (320), na kundi la pili mwaka 2019 walikua wanafunzi (540), na mwaka huu wamehitimu wanafunzi (586), wamefundishwa masomo yanayo endana na umri wao katika fani ya uhadhiri wa Husseiniyya, Fiqhi, Akhlaq na mengineyo”.

Vikafuata vipeperushi kwa anuani isemayo (Shufaa ya Zaharaa a.s) na utenzi usemao (Wahyi-Dhwamiri) pamoja na igizo, mashairi na kisa cha kuzaliwa kwake.

Baada ya hapo washiriki wa mradi wakapewa zawadi pamoja na walimu wao, ukafuata upigaji kura kwa ajili ya kupata washindi wa shindano la kuhifadhi khutuba ya Fadakiyya ya bibi Zaharaa (a.s) lililofanywa siku za nyuma, washindi watatu waliopatikana ni:

  • - Mshindi wa kwanza: Zainabu Abbasi Ali.
  • - Mshindi wa pili: Hanaa Jabaar Muhammad.
  • - Mshindi wa tatu: Taisiri Swalahu Abdulhussein.

Baada ya hapo wahudhuriaji wakaenda kwenye ufunguzi wa maktaba maalum ya idara, ambayo imeratibiwa na watumishi wa idara ya maktaba ya Ummul-Banina (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na maonyesho ya vitabu na kazi za uchoraji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: