Dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) limepambwa kwa mauwa kufuatia mazazi ya Shaabaniyya

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya na idara ya usimamizi wa haram tukufu, Jumatano ya jana jioni wamemaliza kazi ya kupamba dirisha tukufu la malalo ya Abulfadhil Abbasi kwa kuweka mauwa, kama sehemu ya kujiandaa kupokea mwezi mtukufu wa Shabani, na kuadhimisha mazazi matakatifu yaliyo tokea katika mwezi huo.

Kiongozi wa idara ya Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya, Sayyid Hashim Shami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na kauli ya Imamu Swadiq (a.s) isemayo: (Huisheni mambo yetu Mwenyezi Mungu amrehemu atakayehuisha mambo yetu). Tumefanya upambaji wa dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), tumekua tukifanya hivi kila mwaka katika tarehe kama hizi”.

Akaongeza kuwa: “Shughuli hiyo ilifunguliwa kwa kusoma ziara ya mwenye malalo takatifu Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa pamoja na dua, kisha tukaanza kuweka mauwa uzuri, yaliyo pendezesha sehemu hiyo takatifu”.

Naye kiongozi wa idara ya haram Ahmadi Karim Yusufu akasema “Hakika tumekua tukifanya hivi kila mwaka katika kuadhimisha watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani, tumeandaa na kuweka shada 60 za mauwa, tumeweka sehemu ya juu na chini ya dirisha takatifu, mauwa hayo yamewekwa manukato maalum yanayo nukia kwa muda mrefu zaidi”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba kamili ya kupokea mwezi wa Shabani na matukio matukufu ya mwezi huo, kuanzia tukio la kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hussein (a.s) mwezi tatu Shabani na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) mwezi nne na Imamu Sajjaad Zainul-Aabidina (a.s) mwezi tano, na mwisho katika kumbukumbu ya kuzaliwa muokozi wa binaadamu Imamu wa Zama (a.f) mwezi kumi na tano Shabani, bila kusahau kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Ali Akbaru mtoto wa Imamu Hussein (a.s) tarehe kumi na moja ya mwezi huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: