Kituo cha Swidiiqatu-Twahirah (a.s) kinafanya hafla ya usomaji wa Qur’ani kwa wanawake

Maoni katika picha
Kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s) cha harakati za wanawake katika mkoa wa Karbala chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya hafla ya wanawake ndani ya ukumbi wa kituo, iliyo ratibiwa na idara ya shule za Alkafeel za Dini na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya wa kike.

Vikao vya usomaji wa Qur’ani vimeanza tangu siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na vitaendelea hadi mwisho wa mwezi, kila siku asubuhi husomwa juzuu moja kwa mtindo wa kupokezana, wasomaji ni wasichana wenye uwezo mzuri wa kusoma Qur’ani tukufu, wahudumu wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na wageni mbalimbali huhudhuria kwenye vikao hivyo vya usomaji wa Qur’ani.

Maandalizi ya vikao hivi vya usomaji wa Qur’ani yalianza siku nyingi, iliundwa kamati maalum ya kuchagua wasomaji bora, wanaosoma kwa kufuata kanuni za tajwidi.

Kumbuka kuwa ratiba ya mwezi mtukufu wa Ramadhani iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, inavipengele vingi kikiwemo kipengele hiki cha vikao vya usomaji wa Qur’ani tukufu, usomaji wa Qur’ani hauishii kwa wanaume peke yake bali kwa wanawake pia, kwa ajili ya kupata fadhila za mwezi huu mtukufu na baraka zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: