Kufanikiwa upasuaji wa kupandikiza usikivu kwenye sikio la kushoto

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel limefanikiwa kufanya upasuaji wa kupandikiza usikivu kwa mgonjwa aliyekua na tatizo la usikivu.

Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo katika hospitali hiyo, Dokta Turki Yusufu Abdalufu amesema kuwa: “Jopo la madaktari wa hospitali ya Alkafeel limefanikiwa kufanya upasuaji na kupandikiza usikivu wa sikio la kushoto kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka (57)”.

Akabainisha kuwa: “Alikua na tatizo kwenye mfumo wa usikivu wa sikio la kushoto”.

Abdaluuf akasema: “Madaktari na wauguzi wa hospitali ya rufaa Alkafeel wanatoa huduma kwa wagonjwa muda wote”.

Tambua kuwa hospitali ya furaa Alkafeel inatoa huduma bora daima kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa ilivyo navyo na madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya taifa, jambo ambalo limeifanya iweze kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya Alkafeel hualika madaktari bingwa wa maradhi tofauti mara kwa mara, sambamba na kupokea wagonjwa mbalimbali walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: