Baada ya swala ya Adhuhuri ya leo mwezi kumi Muharam mwaka (1444h) sawa na tarehe (9 Agosti 2022m), yameanza matembezi ya waombolezaji ya Towareji ambayo hushiriki mamilioni ya watu.
Matembezi yameanzia eneo la Salaam lililopo umbali wa kilometa tano kutoka haram ya Imamu Hussein (a.s), wanapitia barabara ya Jamhuriyya hadi kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s), kisha wanapitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili hadi kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), chini ya ulinzi mkali na usimamizi wa watumishi wa Ataba mbili tukufu.