Watumishi wa Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) wamegawa zaidi ya sahani za chakula elfu 15 kwa mazuwaru

Maoni katika picha
Kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) katika mkoa wa Karbala chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimegawa zaidi ya sahani za chakula (elfu 15) kwa mazuwaru wakati wa ziara ya Ashura na baada yake, sambamba na maelfu ya chupa za maji ya kunywa.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Adnani Dhaifu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ya kutoa huduma bora kwa mazuwaru wa Ashura, watumishi wa kitengo chetu waliweka mkakati wa kutoa huduma bora kwa kila anayekuja kutembelea sehemu hii tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa huduma zilizotolewa mwaka huu na kitengo chetu ni ugawaji wa chakula kwa mazuwaru, tulianza kugawa chakula mwezi tano Muharam, baada ya kuongezeka idadi ya mazuwaru, tukaendelea hadi baada ya siku ya kumi Muharam, kila siku tulikua tunagawa zaidi ya vifurushi (3000) vya chakula, sambamba na maelfu ya chupa za maji safi ya kunywa”.

Akamaliza kwa kusema: “Tuliweka ratiba ya ugawaji wa chakula, tulichagua muda ambao unakuwa na mazuwaru wengi wanaokuja kutembelea Maqaam takatifu, mwaka huu Maqaam imeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru, tumewapokea na kuwawekea mazingira rafiki ya kufanya ziara na ibada zingine”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: