Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu amekutana na viongozi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Murtadha Dhiyaau-Dini asubuhi ya Jumamosi (20/8/2022m) ametembelea ofisi ya kitengo cha malezi na elimu ya juu, na kufanya kikao na raisi wa kitengo hicho pamoja na wasaidizi wake wa taaluma na mkuu wa shule za Al-Ameed za wavulana na wasichana.

Katibu mkuu amepongeza kazi zinazofanywa na kitengo hicho ikiwa ni pamoja na semina za kujengea uwezo watumishi wake zilizo fanywa kwa watumishi wote wakati wa likizo ya majira ya joto, sambamba na kutoa pongezi nyingi kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana mwakajana.

Akahimiza kuendelea kutekeleza wajibu wao kama wazazi kwenye sekta ya malezi, elimu na idara, waendelee kuwa kiigizo chema, yote hayo yatapatikana kwa kuendelea kufanya kazi kwa weledi.

Ziara hii imefanywa kutokana na umuhimu wa miradi ya malezi na elimu ya juu chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: