Kutoka Karbala.. Makatibu wakuu wa Ataba wamekutana kujadili namna ya kusaidia Atabatu Askariyya

Maoni katika picha
Malalo ya Imamu Hussein (a.s) imeshuhudia mkutano wa makatimu wakuu wa Ataba wakijadili namna ya kusaidia Atabatu Askariyya tukufu na kushirikiana nayo katika kutoa huduma bora kwa mazuwaru.

Katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya tukufu Ustadhi Hassan Rashidi Abaiji amesema “Ataba tukufu za Iraq zinaumuhimu mkubwa hapa nchini, ndio kimbilio salama kwa tabaka zote za raia wa Iraq”.

Kikao kimehusisha makatibu wakuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, pamoja na Atabatu Alawiyya, Kadhimiyya, Askariyya na viongozi wakuu wa mazaru za kishia na Masjidi Kufa tukufu.

Akaongeza kuwa: “Ataba tukufu huhakikisha zinatoa huduma bora kwa mazuwaru wakati wote hususan kwenye ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ikiwa ni pamoja na huduma ya usafiri, malazi, chakula na usalama”.

Akabainisha kuwa “Kikao kimejikita katika kujadili namna ya kusaidia Atabatu Askariyya takatifu, na kushikamana nayo katika kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru”.

Kwa mujibu wa waliokutana, hakika ishara zinaonyesha kuwa ziara ya Arubaini mwaka huu itakuwa na idadi kubwa ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: