Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema, upandaji wa miti kwenye malango ya kuingia Karbala hufanywa na kikosi maalum chenye jukumu la kupanda na kufuatilia maendeleo ya miti hiyo wakati wote wa mwaka.
Kiongozi wa idara ya upandaji wa miti Raad Mughimish Haziraan amekiambia kituo cha Habari kuwa “Kikosi cha watunza bustani (shamba boy) cha Alkafeel, kimeanza kupanda miti kwenye malango yanayoingia katika mji mtukufu wa Karbala kupitia mradi wa upandaji miti unaofanywa na Ataba kwa miaka 11 sasa”.
Akaongeza kuwa “Aina ya miti iliyopandwa ni (Akasiya ya Misri, Albiziya, Saljiniya na Bunisyani nyekundu)”, akafafanua kuwa “Upandaji wa miti hufanywa na kikosi maalum kinacho wajibika kumwagilia na kuchambulia miti hiyo mwaka mzima”.
Kuhusu kazi ya kuchambulia miti akasema kuwa: “Baadhi ya miti huchambuliwa kila mwezi na mingine mwanzoni mwa msimu wa masika na mingine mwanzoni mwa msimu wa kipupwe”.








