Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Jumatano, umefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Swidiqah Twahira Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya kwanza.
Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imehutubiwa na Shekhe Abdullahi Kaabi, ameeleza dhulma alizofanyiwa bibi Zaharaa (a.s) na matukio yaliyo pelekea tukio kubwa linalo umiza.
Majlisi itaendelea kwa muda wa siku tatu, kila siku kutakuwa na mihadhara miwili, mhadhara wa kwanza unatolewa asubuhi na wa pili jioni baada ya swala ya Isha.