Majmaa-Ilmi imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s)

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Fatuma Zaharaa (a.s).

Majlisi hiyo imesimamiwa na idara ya harakati za Qur’ani katika Maahadi ya Qur’ani ya Najafu chini ya Majmaa.

Imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Ali Zubaidi, akafuata Muhammad Ridhwa Jaabir kisha Shekhe Qassim Janabi.

Majlisi hiyo ni sehemu ya harakati za Maahadi katika kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) sambamba na harakati zingine zinazolenga kutoa elimu ya vizito viwili katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: