Kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Alkafeel kimeanza kuandikisha wanafunzi kutoka mikoa yote

Kitivo cha udaktari katika chuo kikuu cha Alkafeel kimeanza kuandikisha wanafunzi kutoka mikoa yote ya Iraq, baada ya kuruhusiwa na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.

Kitivo hicho kimefunguliwa rasmi baada ya kutimiza masharti yote, ikiwa ni bamoja na majengo, maabara, kumbi za madarasa na walimu wenye sifa.

Chuo kikuu cha Alkafeel kinamajengo mazuri katika mji wa Najafu, kinamaabara nzuri zilizojaa mitambo ya kisasa na walimu bobezi, sifa hizo zimewavutia wanafunzi kutoka mikoa yote ya Iraq.

Chuo kinafanya kila kiwezalo kuhakikisha kinakuwa bora hapa nchini, ukizingatia kuwa kipo chini ya bendera ya kimataifa Alkafeel.

Ukubwa wa eneo la chuo ni mita elfu mbili mia mbili na hamsini, jingo lake ni ghorofa sita, lenye ukubwa wa mita za mraba elfu kumi na tatu na mia tano, linahospitali maalum kwa ajili ya kutolea mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi, ili kutoa wahitimu wenye maarifa makubwa katika fani zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: