Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amekutana na mmoja wa wasomaji kutoka mkoa wa Basra ambaye ni mwanafunzi wa mmoja wa walimu wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, bwana Haidari Bazuni.
Rais wa Majmaa Dokta Mushtaqu Ali amesema “Kutokana na malengo makubwa ya kimkakati yaliyopo Atabatu Abbasiyya tukufu, ya ujenzi wa jamii bora, na chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, yanayo husu kusaidia watu wanaosoma Qur’ani kwa mahadhi ya kiiraq, tumeuona usomaji huo kwa bwana Haidari Bazuni, tunaweza kumtoa mbele na walimwengu wote wakaona kisomo chake”.
Akaongeza kuwa “Leo kijana huyu bwana Haidari Bazuni kutokana na juhudi yake ya kutumikia Qur’ani tukufu, amepewa zawadi na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, kwa lengo la kumtia moyo wa kuendelea kushikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu pamoja na kuwatumikia Ahlulbait (a.s)”.
Naye msomaji bwana Haidari Bazuni amesema: “Maneno ya Sayyid Swafi yananisukuma sana katika kuitumikia Qur’ani tukufu na kuendeleza mahadhi ya kiiraq”.