Kwa mahudhurio makubwa ya wanawake.. chuo kikuu cha Al-Ameed kimefanya mhadhara kuhusu changamoto za watoto wa chekechea

Kitivo cha malezi ya msingi kwa wasichana katika chuo kikuu cha Al-Ameed kimetoa mhadhara wa kielimu wenye anuani isemayo (Changamoto wanazopata watoto wa chekechea na mbinu anazoweza kutumia mwalimu wa chekechea).

Mhadhiri wa nadwa hiyo Dokta Zainabu Muhammad Kaatwii amesema, mhadhara umetolewa ndani ya ukumbi wa kitivo katikati ya majengo ya shule za Al-Ameed, umehudhuriwa na kundi kubwa la wanawake waliojadili changamoto za watoto na namna ya kuzitatua.

Akaongeza kuwa, mhadhara umejikita kuhusu umuhimu wa mwalimu wa chekechea na mahitaji yake, ukizingatia kuwa ndiye mwenye jukumu la kumjenga mtoto kimaadili na kielimu.

Mhadhara umewalenga walimu wa chekechea katika shule za Al-Ameed na wanafunzi wao, akasisitiza kuwa chuo kinafanya kila jambo katika kupambana na changamoto zilizopo kwenye jamii na kuangalia namna ya kuzitatua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: