Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya kinaendelea na maandalizi ya awamu ya kwanza ya kongamano la Nabiyyu Rahma katika chuo kikuu cha Mosul.
Kiongozi wa idara ya mahusiano ya vyuo na shule Sayyid Maahir Khaalid amesema “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya ya kudumisha mawasiliano na vyuo vikuu kwa kufanya makongamano na shughuli za kitamaduni, na baada ya kukubaliana na uongozi wa chuo kikuu cha Mosul kuwa mwenyeji wa kongamano hili, tulianza moja kwa moja kufanya maandalizi ya kongamano”.
Akaongeza kuwa “Miongoni mwa maandalizi hayo tumetembelea uongozi mkuu wa chuo na kukutana na rais wa chuo, tumejadili kwa pamoja maandalizi yanayo fanywa na kukubaliana shughuli zitakazo fanywa kwenye kongamano litakalo dumu kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 21 Februari”.
Rais wa chuo Dokta Qais Ahmadi ameshukuru Atabatu Abbasiyya kwa kusimamia tukio hilo muhimu litakalo fanywa hapa chuoni, aidha amepongeza msaada mkubwa unaotolewa na Ataba kwa wanafunzi hapa chuoni na nchini kwa ujumla.