Atabatu Abbasiyya inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Bibi Zainabu (a.s).

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya, inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha jabali wa Subira Bibi Zainabu (a.s).

Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia majlisi za asubuhi na jioni kupitia mradi wa Ummul-Banina (a.s), zinazo hudhuriwa na watumishi wa malalo takatifu na kundi la mazuwaru.

Mhadhiri Sayyid Nuuri Baaqir anazungumza katika majlisi ya asubuhi, anaeleza historia ya Bibi Zainabu (a.s) na namna alivyo simama imara kumnusuru Imamu Hussein (a.s), akahimiza umuhimu wa kushikamana na mwenendo wake mtukufu.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya maombolezo hayo, imetangaza msiba na imewekwa mapambo meusi pamoja na vitambaa vilivyo andikwa jumbe mbalimbali zinazotaja dhulma alizofanyiwa Bibi Hauraa (a.s).

Ataba tukufu zimejiandaa kupokea mawakibu za waombolezaji wanaokuja kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na msiba huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: