Kuingia kwa mwezi wa Shabani.. Kukamilisha ushonaji wa vitambaa vya kuadhimisha mazazi ya Maimamu watakasifu

Watumishi wa kitengo cha zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya, wamekamilisha ushonaji wa vitambaa vya kuadhimisha mazazi ya Maimamu watakasifu (a.s) katika mwezi wa Shabani.

Kiongozi wa idara ya ushonaji na kudarizi Sayyid Abduzuhra Daud amesema kuwa “Idara yetu imemaliza kushona na kudarizi vitambaa maalum vya kuadhimisha kuzaliwa kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) vitakavyo wekwa kwenye maeneo tofauti ya Ataba tukufu”.

Akaongeza kuwa “Kazi ya kushona vitambaa hivyo imefanywa na watumishi wa idara ya ushonaji, kupitia cherehani za mikono na kompyuta”.

Akabainisha kuwa “Vitambaa vyote vilivyo andaliwa vitawekwa ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia maadhimisho ya kuzaliwa Maimamu watakasifu (a.s) katika mwezi wa Shabani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: