Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza majina ya washindi wa shindano la (watukufu waliozaliwa katika mwezi wa Shabani) awamu ya tatu mahsusi kwa kuzaliwa Imamu Zainul-Aabidina (a.s).
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umesema kuwa, zawadi zitatolewa katika eneo la mlango wa Kibla mbele ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) saa moja jioni siku ya Jumamosi tarehe (25/2/2023).
Awamu ya kwanza ilikuwa mahsusi kwa ajili ya mazazi ya Imamu Hussein (a.s), na awamu ya pili ikawa mahsusi kwa mazazi ya Abulfadhil Abbasi (a.s).