Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kila iwezalo katika kuhudumia watu wanaokuja kufanya zaira ya nusu ya mwezi wa Shabani na kuadhimisha mazazi ya Imamu Mahadi (a.f).
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi amesema “Huduma zilizotolewa na watumishi wa Ataba kwa mazuwaru huongezeka mwaka baada ya mwaka, bila kusahau ulinzi wa amani, ubebaji wa mazuwaru na kuwapeleka hadi kwenye haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma, tunafanya kazi kwa kushirikiana na Atabatu Husseiniyya, ofisi ya mkuu wa mkoa na polisi wa mkoa wa Karbala”.
Kwa mujibu wa makamo katibu mkuu amesema “Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimefanya makubaliano ya kisheria na mawakibu (834) zilizoshiriki mwaka huu kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru, ikiwa ni pamoja na chakula na vinywaji, jumla ya sahani za chakula (287,417) zimetolewa, bila kusahau kikosi cha wapiganaji kilichotoa sahani (18,000), jumla itakuwa ni (305,417), huku katoni za maji (1,500,000) zikitolewa bure kutoka kiwanda cha Alkafeel”.
Akafafanua kuwa “Idadi ya wahudumu wa kujitolea imefika (3,026) huku kikosi cha Abbasi cha wapiganaji kikitoa wahudumu wa kujitolea (1000, hivyo jumla ya wahudumu wa kujitoea ni (4,026), vikundi vya wahudumu wa kujitolea vipo (49)”.
Kuhusu vyombo vya habari amesema kuwa, jumla ya taasisi (15) zimeshiriki kutangaza ziara hii kupitia wanahabari (40).
Akaendelea kusema kuwa “Upande wa matibabu, tuliandaa gari (10) za wagonjwa na vituo (9) vya kutolea huduma za afya, idadi ya wato huduma za dharura walikuwa (275) huku madaktari na wauguzi walioshiriki kutoa huduma katika ziara hii wakiwa (270)”.
Kwa mujibu wa maelezo ya Ahmadi “Kitengo cha usafiri kiliandaa gari (130) aina ya Kosta (9) basi kubwa, (7) gari za kubeba maji (6) gari za kuvuta na gari (19) ndogo, hivyo jumla ya gari zilizo shiriki ni (171)”.