Kitengo cha habari kimefanya maonyesho ya nafasi ya wasubiriaji katika zama za qhaiba kubwa

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya maonyesho yanayohusu nafasi ya wasubiriaji katika zama za qhaiba kubwa kupitia program ya (waulizeni wanaojua).

Mkuu wa maktaba ya Ummul-Banina (a.s) ya wanawake, chini ya Atabatu Abbasiyya ameonyesha nafasi ya wanaosubiri katika zama za qhaiba kubwa kupitia program ya (waulizeni wanaojua).

Mkuu wa maktaba ya Ummul-Banina (a.s) bibi Nuru Ali amesema “Wiki hii tumeweka utaratibu wa kusoma kitabu cha (katika zama na kusubiri) kilicho andikwa na Shekhe Hussein Abduridhwa Asadii katika ratiba inayoendelea ndani ya Sardabu ya Imamu Alkaadhim (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Tumeongea kuhusu umuhimu wa kusoma sambamba na maelezo ya kitabu yanayo himiza wajibu wa wanaomsubiri Imamu (a.f), kitabu kina kurasa (224) na makala (114) zinazo fafanua fitina zitakazotokea kabla ya kudhihiri Imamu na mambo yatakayotokea baada ya kudhihiri kwake”.

Akabainisha kuwa “Moja ya Makala zilizopo kwenye kitabu imeeleza nafasi ya mwanamke katika kuandaa mazingira ya kudhihiri Imamu (a.f), imeandikwa kwa nukta muhimu ikiwemo ya malezi ya watoto na kujistiri”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: