Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimehitimisha ratiba ya kitamaduni kwa wageni kutoka kitivo cha uhandisi katika chuo kikuu cha Mosul.
Kiongozi wa idara ya mahusiano Sayyid Maahir Khalidi amesema “Kupitia ratiba ya kila wiki inayohusu walimu na wanafunzi wa vyuo, Atabatu Abbasiyya imepokea ugeni kutoka chuo kikuu cha Mosul na kuwapangia ratiba maalum yenye vipengele vingi”.
Akaongeza kuwa “Ratiba ilifunguliwa kwa kufanya ziara katika Ataba mbili tukufu na kutembelea vitengo vya Atabatu Abbasiyya, ikiwa ni pamoja na kutembelea makumbusho ya Alkafeel, kituo cha kukarabati nakala-kale, maktaba kuu na kusikiliza mihadhara miwili iliyotolewa na Ustadhi Jaasim Saidi na mada kuhusu uhakika wa Dini iliyotolewa na Shekhe Haarith Daahi”.
Khalidi akafafanua kuwa “Siku ya pili tumetembelea kituo cha kusafisha mafuta, na kupewa maelekezo kuhusu kituo hicho na umuhimu wake, na siku ya tatu tukatembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya zikiwemo shule za Al-Ameed, maegesho ya Alkafeel na shirika la Aljuud”.
Wageni wameonyesha furaha kubwa na wamepongeza miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wakasema kuwa inaumuhimu mkubwa katika kuhudumia raia.